Maandamano ya kupinga ukiukaji wa usitishaji vita Gaza yafanyika nchini Sweden
https://parstoday.ir/sw/news/world-i139486-maandamano_ya_kupinga_ukiukaji_wa_usitishaji_vita_gaza_yafanyika_nchini_sweden
Maandamano makubwa ya kupinga ukiukaji wa usitishaji vita Gaza yamefanyika nchini Sweden yakilaani pia jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.
(last modified 2026-06-28T10:27:23+00:00 )
Jun 28, 2026 09:47 UTC
  • Maandamano ya kupinga ukiukaji wa usitishaji vita Gaza yafanyika nchini Sweden
    Maandamano ya kupinga ukiukaji wa usitishaji vita Gaza yafanyika nchini Sweden

Maandamano makubwa ya kupinga ukiukaji wa usitishaji vita Gaza yamefanyika nchini Sweden yakilaani pia jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Mamia ya watu waliandamana huko Stockholm, mji mkuu wa Uswidi, siku ya Jumamosi kupinga kuendelea kwa mashambulizi ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza na vikwazo vilivyowekwa vya kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwenye ukanda huo.

Kulingana na Shirika la Habari la Quds (Qudsna), maandamano hayo yamefanyika kwa mwaliko wa mashirika kadhaa ya kiraia katika Uwanja wa Odenplan.

Washiriki, wakiwa na mabango, walilaani mashambulizi dhidi ya Gaza, mabomu dhidi ya shule na hospitali, na mauaji ya watoto wa Kipalestina.

Aidha waandamanaji hao wametaka kusitishwa mara moja mashambulizi hayo, kukomeshwa vikwazo vya kuingia chakula, na kuheshimu utawala wa Kizayuni makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosainiwa Oktoba 10, 2025.

Wakati huo huo mji mkuu wa Ireland, Dublin, umeshuhudia kufanyika kwa wakati mmoja shughuli mbalimbali za wananchi na matukio ya michezo yaliyolenga kuunga mkono Palestina na kupinga kuanzishwa uhusiano wa kimichezo na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Washiriki wa kampeni hiyo walisisitiza kuwa, hatua hiyo ni sehemu ya shinikizo la wananchi na wanamichezo la kushinikiza kusitishwa ushiriki wa timu za Israel katika mashindano ya kimataifa. Walisema kuwa, kuendelea ushiriki wa timu hizo huku vita dhidi ya Ukanda wa Gaza vikiendelea ni aina ya kuhalalisha kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa kivamizi, jambo ambalo wanapinga.