Iran: Tunao uwezo wa kuishambulia Israel kwa 'darzeni' za operesheni sawa na "Ahadi ya Kweli"
Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema Iran inao uwezo wa kuteketeza 'darzeni' za operesheni za kulipiza kisasi sawa na "Operesheni ya Ahadi ya Kweli" iliyotekeleza mwezi Aprili kulenga maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Palestina unayoikalia kwa mabavu.

Operesheni hiyo ya pili ya Ahadi ya Kweli ilifanyika katika kukabiliana na ukhabithi mbaya zaidi uliofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran na mataifa mengine ya eneo hili, ukiwemo wa mauaji ya kigaidi ya Kiongozi wa Hamas Ismail Haniyah, Kiongozi wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah, na Abbas Nilforoushan, kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
Kwa mujibu wa Rezaei, Waziri wa Ulinzi amesema, asilimia 90 ya makombora yaliyorushwa katika Operesheni ya Ahadi ya Kweli II yaligonga shabaha zilizokusudiwa, lakini utawala wa Kizayuni ulijaribu kuchuja na kudhibiti ukweli halisi kuhusu operesheni hiyo.
Wakati huo huo, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amezungumzia mashambulizi yaliyofanywa wiki iliyopita na utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya ulinzi katika mikoa ya Tehran, Khuzestan, na Ilam.
Amesema, mashambulizi hayo hayakuweza kuleta madhara makubwa katika mzunguko wa utengenezaji makombora na mfumo wa ulinzi nchini na akaongeza kuwa madhara yote yaliyosababishwa na shambulio hilo yamesawazishwa.
Katika upande mwingine, Msemaji wa Kamati ya Bunge ya usalama wa Taifa na Sera za Nje Rezaei amebainisha kuwa katika kikao hicho cha jana baadhi ya wabunge walilalamikia hatua ya serikali za Jordan na Iraq kuruhusu anga za nchi zao kutumiwa na utawala wa Israel kufanya mashambulizi dhidi ya Iran.../