Araghchi: Magenge ya ukufurishaji hayawezi kufanya lolote mbele ya Muqawama
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119584-araghchi_magenge_ya_ukufurishaji_hayawezi_kufanya_lolote_mbele_ya_muqawama
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, harakati za kidiplomasia na mapambano kwenye medani ya vita ni vitu viwili visivyotenganishika na kwamba nguvu za kidiplomasia zinategemea nguvu za kwenye medani ya mapambano.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Dec 01, 2024 08:04 UTC
  • Araghchi: Magenge ya ukufurishaji hayawezi kufanya lolote mbele ya Muqawama

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuwa, harakati za kidiplomasia na mapambano kwenye medani ya vita ni vitu viwili visivyotenganishika na kwamba nguvu za kidiplomasia zinategemea nguvu za kwenye medani ya mapambano.

Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo kwenye hafla ya kuadhimisha Siku ya Jeshi la Majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusisitiza kuwa magenge ya kigaidi na ukufurishaji hayawezi kufanya lolote mbele ya nguvu za kambi ya Muqawama. 

Vilevile amesema kuwa udiplomasia ni njia yenye gharama ndogo na ndiyo njia bora ya kufikia malengo lakini uhakika utabakia pale pale kwamba nguvu za kidiplomasia za kila nchi zinatengemea nguvu za ndani ya nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia amesema kuwa, magenge ya ukufurishaji na mabwana zao wanapaswa kuelewa kuwa, vikosi vya kambi ya Muqawama vinaendesha mapambano kwa ajili ya kulinda mataifa yao, ukombozi wa nchi zao na kuwaletea heshima na hadhi watu wao, wakati magenge ya ukufurishaji ni vibaraka wa madola ya kibeberu na yanafanya kinyume na inavyofanya kambi ya Muqawama, hivyo magenge ya ukufurishaji hayawezi kukabiliana na nguvu za kila upande za vikosi vya Muqawama.

Vilevile amesema kuwa, imethibitika kwamba, Marekani, utawala wa Kizayuni na magenge ya ukufurishaji wanashirikiana kikamilifu katika kukabiliana na kambi ya Muqawama na huo ni uhakika ambao umethibitishwa kihistoria na kwa ushahidi madhubuti.