Araghchi: Kuna mipango ya pamoja ya Israel na Marekani kufanya ugaidi Syria
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119652-araghchi_kuna_mipango_ya_pamoja_ya_israel_na_marekani_kufanya_ugaidi_syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kuna uratibu kamili kati ya utawala wa Kizayuni, Marekani na makundi ya kigaidi, na mwenendo wa matukio unaashiria uratibu na mpangilio wa magaidi."
(last modified 2024-12-03T03:50:00+00:00 )
Dec 03, 2024 03:50 UTC
  • Araghchi: Kuna mipango ya pamoja ya Israel na Marekani kufanya ugaidi Syria

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: "Kuna uratibu kamili kati ya utawala wa Kizayuni, Marekani na makundi ya kigaidi, na mwenendo wa matukio unaashiria uratibu na mpangilio wa magaidi."

Seyed Abbas Araghchi amesema hayo katika mahojiano na televisheni  na kubainisha kwamba, katika safari yake huko Damascus, ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa uungaji mkono kamili na wa uhakika kwa serikali ya Syria na watu wake ulifikishwa kwa Rais Bashar Assad.

Waziri Araghchi ameeeleza kuwa, kama ambavyo wakati wa mashambulio ya utawala wa Baath dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu Damascus ilikuwa pamoja na Iran, Tehran pia itakuwa upande wa Damascus kkatika kipindi hiki.

Akizungumzia safari yake ya mjini Ankara, Araghchi pia amesema: Kuna maafikiano kati ya Iran na Uturuki kuhusu suala kwamba, Syria isiwe mahali pa magaidi, kwa sababu suala hili litasababisha vita katika eneo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran pia ametangaza kufanyika kwa mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Iran, Russia na Uturuki wiki ijayo mjini Doha, Qatar kwa minajili ya kujadili kadhia ya Syria.