Mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu wa Iran watangaza ongezeko la akiba
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119672-mgodi_mkubwa_zaidi_wa_dhahabu_wa_iran_watangaza_ongezeko_la_akiba
Mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu wa Iran  una akiba zaidi ambayo imebainika baada ya uchunguzi katika mgodi huo ulio kaskazini magharibi mwa Iran.
(last modified 2024-12-03T23:52:50+00:00 )
Dec 03, 2024 23:52 UTC
  • Mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu wa Iran watangaza ongezeko la akiba

Mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu wa Iran  una akiba zaidi ambayo imebainika baada ya uchunguzi katika mgodi huo ulio kaskazini magharibi mwa Iran.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Zarshouran Mohammad Parvin amesema mashapo ya madini ya dhahabu yaliyothibitishwa katika mgodi huo yameongezeka kutoka tani milioni 27 hadi 43 milioni kulingana na matokeo ya shughuli za hivi karibuni za uchunguzi.

Parvin amesema ongezeko hilo linapandisha rasilimali ya dhahabu inayochimbwa katika mgodi huo na hivyo kuimarisha uwekezaji zaidi na ajira katika jimbo la Azerbaijan Magharibi mwa Iran na maeneo yanayoizunguka.

Zarshouran inamilikiwa na kampuni ya madini ya Iran ya IMIDRO. Ni mgodi mkubwa zaidi wa dhahabu katika eneo la Asia Magharibi na ndio mzalishaji mkubwa zaidi wa baa za dhahabu nchini Iran na pato la kila mwezi la karibu kilo 100 .

Sekta ya madini Iran inazidi kuimarika pamoja na kuwepo vikwazo vya madola ya Magharibi hasa Marekani. Iran sasa inajitegemea katika teknolojia na mashine za uchimbaji madini na tayari imeshatia saini mapatano na nchi kadhaa za Afrika katika sekta ya madini.