Baqaei: Iran inahuisha sentrifyuji zaidi za kisasa katika fremu ya NPT
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i119996-baqaei_iran_inahuisha_sentrifyuji_zaidi_za_kisasa_katika_fremu_ya_npt
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa uamuzi wa karibuni wa Tehran wa kuhuisha sentrifyuji zaidi za kisiasa umechukuliwa katika fremu ya haki ya nchi wanachama wa mkataba wa NPT na kwa kutolewa taarifa kabla na kwa usimamizi wa Wakala wa kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).
(last modified 2024-12-11T03:50:03+00:00 )
Dec 11, 2024 03:50 UTC
  • Baqaei: Iran inahuisha sentrifyuji zaidi za kisasa katika fremu ya NPT

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa uamuzi wa karibuni wa Tehran wa kuhuisha sentrifyuji zaidi za kisiasa umechukuliwa katika fremu ya haki ya nchi wanachama wa mkataba wa NPT na kwa kutolewa taarifa kabla na kwa usimamizi wa Wakala wa kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Troika ya Ulaya inayoundwa na Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zimekariri madai ya kisiasa kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran inayofanyika kwa malengo ya amani katika radiamali yao kwa ripoti ya karibuni ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki kuhusu Iran kuzidisha uzalishaji wa urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60. 

Nchi za Troika ya Ulaya bila ya kuashiria kuwa zimeshindwa kutekeleza ahadi na majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA zimedai kuwa hatua za Iran zitayaacha tupu makubaliano ya JCPOA na kuzidisha akiba ya urani iliyorutubishwa ya nchi hii ambayo haiwezi kuhalalishwa kwa namna yoyote kuwa ni ya malengo ya kiraia.

Ismail Baqaei msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekadhibisha madai haya ya Troika ya Ulaya yaliyotolewa kupitia taarifa ya pamoja ya wasemaji wa Wizara za Mambao ya Nje za Ufaransa, Ujerumani na Uingereza kuhusiana namatukio ya karibuni ya miradi ya nyuklia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yenye malengo ya kiraia na kusema: Iran ambayo ni nchi mwanachama wa  IAEA inayowajibika imethibitisha dhamira yake ya kushirikiana na wakala huo, na mapatano yaliyofikiwa katika ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA mjini Tehran mwezi Novemba pia yanathibitisha suala hilo. 

Rafael Grossi katika ziara yake mjini Tehran hivi karibuni 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema inasikitisha kuona kuwa nchi tatu hizo za Ulaya zinasisitiza kuhusu mtazamo wao haribifu na kinzani na kupasisha azimio dhidi ya Iran bila ya kutilia maani mafanikio ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA hapa Tehran ambayo yanaweza kuwa msingi wa kuimarisha ushirikiano katika siku zijazo.