Araqchi asisitiza kuendeleza mashauriano kati ya Iran na Japan
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i120212-araqchi_asisitiza_kuendeleza_mashauriano_kati_ya_iran_na_japan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuendeleza mashauriano kati ya pande mbili kuhusu masuala ya amani na utulivu katika eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2024-12-16T03:57:38+00:00 )
Dec 16, 2024 03:57 UTC
  • Araqchi asisitiza kuendeleza mashauriano kati ya Iran na Japan

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuhusu umuhimu wa kuendeleza mashauriano kati ya pande mbili kuhusu masuala ya amani na utulivu katika eneo la Asia Magharibi.

Waziri ameeleza haya katika mazungumzo na Funakoshi Takehiro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan jana Jumapili hapa Tehran.  

Katika mazungumzo hayo, Sayyid Abbas Araqchi ameashiria uhusiano mzuri na wa kirafiki kati ya nchi mbili za Iran na Japan na akaunga mkono kufanya mashauriano na Japan kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala ya kikanda na kimataifa. 

Iran na Japan zimekuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu 

Araqchi ameongeza kuwa: Kuendelea kwa mashauriano haya ni muhimu kwa kuzingatia matukio ya hivi karibuni  katika eneo la Magharibi mwa Asia hususan huko Syria, na wasiwasi wa pamoja wa nchi mbili  hizi kuhusu hali ya amani na usalama endelevu katika eneo . 

Kwa upande wake Funakoshi Takehiro, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan  ameashiria uhusiano wa siku nyingi na wa kirafiki wa Iran na Japan na kusema kuna udharura wa kuendeleza mashauriano kwa ajili ya kustawisha uhusiano wa pande mbili na kusaidia kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa.