Baqaei: Iran inataka kuimarisha uhusiano na Venezuela
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121334-baqaei_iran_inataka_kuimarisha_uhusiano_na_venezuela
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemtakia mafanikio Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na kusisitiza kuwa Iran ina hamu ya kushirikiana na serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Venezuela kwa manufaa ya mataifa mawili ili kuimarisha uhusiano mkubwa kati ya pande mbili.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 12, 2025 04:32 UTC
  • Baqaei: Iran inataka kuimarisha uhusiano na Venezuela

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amemtakia mafanikio Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na kusisitiza kuwa Iran ina hamu ya kushirikiana na serikali iliyochaguliwa na wananchi ya Venezuela kwa manufaa ya mataifa mawili ili kuimarisha uhusiano mkubwa kati ya pande mbili.

Ismail Baqaei ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, Twitter ya zamani akisema kuwa: Iran inampongeza Nicolas Maduro kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kibolivari ya Venezuela .

Hafla ya kuapishwa Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro 

Baqaei ameongeza kuwa: Iran inamtakia Maduro mafanikio katika kuitumikia nchi na wananchi wa Venezuela, na inatangaza mshikamano wake na wananchi na serikali ya Caracas katika kukabiliana na uingiliaji kati na vikwazo vya upande mmoja na haramu vya Marekani.

Nicolas Maduro aliapishwa Ijumaa iliyopita kuwa Rais wa Venezuela kwa muhula  wa tatu wa miaka sita. 

Kufuatia kufanyika uchaguzi wa Rais wa Venezuela Julai 28, mwaka jana, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimtangaza Maduro kuwa mshindi kwa kupata asilimia asilimia 51.95 ya kura akifuatiwa na mpinzani wake, Edmundo Gonzalez alipata asilimia 43.18.