Imam Khamenei: Mustakabali utaonyesha ni nani amedhoofika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121762-imam_khamenei_mustakabali_utaonyesha_ni_nani_amedhoofika
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja kudhoofika kwa nchi kuwa ni dhana potofu na njozi ya maadui.
(last modified 2026-05-06T11:35:21+00:00 )
Jan 22, 2025 09:51 UTC
  • Imam Khamenei: Mustakabali utaonyesha ni nani amedhoofika

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ametaja kudhoofika kwa nchi kuwa ni dhana potofu na njozi ya maadui.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa,  fikra ya kudhoofika nchi ya Iran ni dhana potofu na ndoto za alinacha za maadui.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika kikao chake na mamia ya wajasiriamali, wawekezaji na wanaharakati wa sekta ya kiuchumi ya Iran na kubainisha kwamba, mustakabali ndio utakaoonyesha ni nani amedhoofika.

Imam Khamenei ametanabahisha kwamba, hata Saddam alianzisha uchokozi na uvamizi dhidi ya Iran kwa wazo la kuidhoofisha Iran, na Rais wa wakati huo wa Marekani Ronald Reagan akampa msaada mkubwa sana kwa wazo hilo hilo, lakini hatimaye wawili hao na makumi wengine wenye kuota ndoto za alinacha waliangamia na Jamhuri ya Kiislamu ilikua siku baada ya siku, na kwa fadhila na baraka za Mwenyezi Mungu, uzoefu huu unaweza kukaririwa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alipokutana na mamia ya wajasiriamali, wawekezaji na wanaharakati wa sekta ya kiuchumi ya Iran

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, kuweko katika jumuiya  kama vile BRICS  ni jambo muhimu.

Ayatullah Khamenei ameashiria ulazima wa maafisa wa kidiplomasia wa Iran kutumia vyema fursa hii adhimu na kuongeza: Mfumo wa kifedha wa BRICS, unaowezesha kubadilishana fedha na sarafu za nchi wanachama ni uwezo na fuursa muhimu.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei ametaja usitishaji vita na ushindi wa Gaza kuwa ni ishara tosha ya kutimia utabiri wa kuwa hai na kuendelea kuwa hai muqawama.

Aidha amesema: Kinachotokea mbele ya macho ya ulimwengu ni mithili ya hadithi na simulizi kwamba jeshi kubwa la kivita kama Marekani limepuuza maana ya ubinadamu na likatoa mabomu ya kuvunja mawe na kuupatia utawala katili na wa umwagaji damu wa Kizayuni, na utawala huo ukashambulia kwa mabomu watoto  15,000 katika nyumba zao na hospitali lakini ushindwe kufikia malengo yake.