Maneva makubwa ya wanamaji wa SEPAH yanafanyika Lango Bahari la Hormoz
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121902-maneva_makubwa_ya_wanamaji_wa_sepah_yanafanyika_lango_bahari_la_hormoz
Maneva makubwa ya kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) yanafanyika katika Ghuba ya Uajemi na katika Lango Bahari la Hormoz.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Jan 25, 2025 22:52 UTC
  • Maneva makubwa ya wanamaji wa SEPAH yanafanyika Lango Bahari la Hormoz

Maneva makubwa ya kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) yanafanyika katika Ghuba ya Uajemi na katika Lango Bahari la Hormoz.

Admeri Alireza Tangsiri, Kamanda wa kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) amesema kuwa, manuva hayo ya kijeshi yalianza siku ya Ijumaa katika Ghuba ya Uajemi na katika Lango Bahari la Hormoz.

Akifafanua zaidi kuhusiana na manuva hayo ya kijeshi Admeri Alireza Tangsiri  amesema, maonyesho haya ya nguvu ya vikosi vinavyoshiriki katika zoezi hili ni sehemu ndogo sana ya uwezo wa Jeshi la Wanamaji la SEPAH.

Admeri Tangsiri amesema, ujumbe wa manuva hayo ya kijeshi ni amani na urafiki kwa nchi jirani na kukabiliana na uvamizi wowote wa vikosi vya nje vya kanda na kusisitiza: Zoezi hili linaonyesha uwezo wetu wa kuimarisha usalama katika eneo.

Sambamba na kusisitiza uimarishwaji wa vipengele vya vita vya majini katika maneva ya kikosi cha Wanamaji cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH), alitangaza kuweko matumizi ya vifaa vipya, vikiwemo vyombo vya mwendo wa kasi, makombora ya kutoka ufukweni hadi baharini.

Licha ya kuweko vikwazo vya kidhalimu, lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ikitegemea wataalamu wake wa ndani imefanikiwa kupiga hatua kubwa mno katika uga wa silaha, ulinzi na kujihami.