Meja Jenerali Salami: Kikosi cha Quds kimemkaba adui maidanini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i122290-meja_jenerali_salami_kikosi_cha_quds_kimemkaba_adui_maidanini
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Kikosi cha Quds cha jeshi hilo kimemmaliza adui kwenye medani za mapambano na kumdidimiza.
(last modified 2025-02-03T23:23:42+00:00 )
Feb 03, 2025 23:23 UTC
  • Meja Jenerali Salami: Kikosi cha Quds kimemkaba adui maidanini

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Kikosi cha Quds cha jeshi hilo kimemmaliza adui kwenye medani za mapambano na kumdidimiza.

Meja Jenerali Hossein Salami amebainisha hayo akisema: "sehemu ndogo ya uwezo wetu imeweza kubadilisha mlingano wa nguvu, na makombora yetu  yanaweza kutoa kipigo katika kila nukta ya maslahi ya adui  wakati wowote ule tena kwa ukubwa na usahihi wa hali ya juu katika eneo hili."

Kamanda Salami amesisitiza kuwa: Meli za jeshi la IRGC zinaweza kukabiliana na adui popote pale baharini, na maafisa wa Marekani wamekiri kuhusu uwezo wa jeshi letu la wanamaji katika eneo la Ghuba ya Uajemi. 

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameashiria kutunguliwa ndege zisizo na rubani za adui, operesheni za ahadi ya kweli na mfano wa hayo, na kusisitiza kwamba, mafanikio hayo yametufanya kuheshimika na kuaminika.  Amesema, Kikosi cha Quds cha IRGC kimemkaba adui kwenye medani na kumdidimiza na tumeandaa uwanja wa vita kila mahali dhidi ya adui.