Kamanda: Jeshi la Iran linabadilisha mbinu za kukabiliana na vitisho
-
Ndege isiyo na rubani ya Iran iliyopewa jina la\\\'Gaza\\\'
Kamanda mwandamizi wa Iran amesema Iran itabadilisha mbinu na mikakati yake ya kijeshi ili kukabiliana na vitisho vinavyobadilika. Kamanda wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Jeshi la Iran, Brigedia Jenerali Alireza Sabahi-Fard, ameyasema hayo Jumamosi na kuongeza kuwa maadui na wavamizi hawawezi kufikia anga ya Iran.
Sabahi-Fard amewaambia makamanda waandamizi na wasimamizi wa Kikosi cha Ulinzi wa Anga kwamba:"Mabadiliko katika mbinu na mikakati yapo kwenye ajenda kwa mujibu wa vitisho vya sasa."
Aliongeza kuwa mabadiliko katika mbinu na mikakati ya Iran yatawachanganya maadui kwa hakika, akibainisha kuwa Kikosi cha Ulinzi wa Anga cha Iran kinafuatilia mkakati huu.
Akizungumzia mipango ya kuboresha uwezo wa kikosi hicho, aliongeza, “Nguvu ya nchi yetu kwa sasa ni mwiba katika koo za maadui.”
Wakati wa mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya Zolfaghar 1403 ya Jeshi la Iran yaliyofanyika kusini mwa nchi mwezi uliopita, kulifanyiwa majaribio yaliyofana ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Jeshi la Iran wa 15 Khordad na droni ya mashambulizi ijulikanayo kama Arash.
Waangalizi wanasema operesheni hiyo ilionyesha maendeleo ya Iran katika teknolojia ya droni na uwezo wake wa kufanya mashambulizi ya masafa marefu kwa usahihi wa hali ya juu, jambo linaloimarisha zaidi uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo katika kanda.
Mazoezi haya, ambayo yalikuwa na lengo la ili kuiga hali halisi za vita, yanaendelea kuonyesha utayari wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika ulinzi wa anga na kujitolea kwake kudumisha mtandao madhubuti na jumuishi wa ulinzi kwa ajili ya kulinda usalama wa taifa lake, wanasema waangalizi.