Ayatullah Khatami: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utamfanya adui ajute
(last modified Fri, 13 Jun 2025 12:53:58 GMT )
Jun 13, 2025 12:53 UTC
  • Ayatullah Khatami: Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran utamfanya adui ajute

Khatibu wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran ameeleza kuwa, kukabiliana na adui na kupambana na mvamizi na dhalimu ni miongoni mwa mafundisho ya Ghadir na akasema: "Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu, mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu utamfanya adui ajutie."

Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami amesema hayo katika khutba zake za Sala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran ambapo akizungumzia jinai ya kigaidi ya utawala wa Kizayuni wa mauaji ya watoto amesema: "Hadi saa tisa usiku wa kumakia leo, nilikuwa nimepanga kutoa khutba za Sala ya Ijumaa kuhusu Ghadir, lakini kwa shambulio la kigaidi la jinai la Kizayuni na kuua utawala wa Kizayuni, nimeamua kuzungumzia jibu lisilo na shaka la Iran kwa utawala wa Kizayuni na vita dhidi ya maaudui kama mafundisho ya Ghadir."

Akizungumzia kuuawa shahidi kundi la makamanda wa kijeshi, wanasayansi na watu wasio na ulinzi wa nchi hii katika shambulio la kigaidi lililofanywa leo asubuhi na utawala wa Kizayuni, khatibu wa muda  wa Sala ya Ijumaa mjini Tehran amesisitiza kuwa: "Tutasimama pamoja na mashahidi waliouawa shahidi leo katika shambulio hili la kijinai hadi pumzi yetu ya mwisho na hadi tone la mwisho la damu, na Mwenyezi Mungu akipenda, kama ilivyokuwa katika mitihani na majaribu mengine, taifa kubwa la Iran litavuka salama pia mtihani huu.

Khatibu wa Sala ya Ijumaa aidha amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu kali na kumfanya adui ajute kwa uchokozi wake.