SEPAH: Wanaopanga kuangamiza Gaza wanatafuta kuumeza ulimwengu wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i129078
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limetahadharisha kuwa, makundi yanayopanga mauaji ya halaiki huko Gaza hayaishii tu katika kuwaangamiza wananchi wa Palestina, bali yanalenga pia kuyameza maeneo tajiri na ya kistratijia ya Ulimwengu wa Kiislamu.
(last modified 2025-08-03T02:27:11+00:00 )
Aug 03, 2025 02:27 UTC
  • SEPAH: Wanaopanga kuangamiza Gaza wanatafuta kuumeza ulimwengu wa Kiislamu

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limetahadharisha kuwa, makundi yanayopanga mauaji ya halaiki huko Gaza hayaishii tu katika kuwaangamiza wananchi wa Palestina, bali yanalenga pia kuyameza maeneo tajiri na ya kistratijia ya Ulimwengu wa Kiislamu.

Taarifa ya SEPAH imeeleza kuwa, hatua hizo ni sehemu ya mradi mpana wa kujitanua unaolenga usalama na rasilimali za umma wa Kiislamu.

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limebainisha katika taarifa yake kwamba, muqawama na kusimama kidete wananchi wa Palestina huko Gaza hii leo katika kukabiliana na mauaji ya kimbari na jinai za Wazayuni, ni ushahidi wa dhamira ya watu hao kwa malengo ya kuikomboa Palestina na Baytul-Muqaddas, na kuendelea kwao na njia ya shahidi mkubwa Ismail Haniyeh - mkuu wa zamani wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas na mashahidi wengine.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: "Kushadidi jinai za utawala wa Kizayuni kwa kuwanyima wakazi wanaodhulumiwa wa Gaza mahitaji ya kimsingi kabisa ya maisha yakiwemo maji, chakula na dawa, ni ukiukwaji wa wazi wa haki za binadamu na sheria za kimataifa, na unaweza kuhesabiwa kuwa ni aina mpya ya mauaji ya kimbari."

Taarifa hiyo iliendelea kusema: "Uhalifu huo wa kinyama unafanywa katika hali ya kimya cha kutatanisha cha kimataifa na ushirikiano wa baadhi ya nchi za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu. Jambo hili limepelekea kuongezeka kwa maandamano ya kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni, na hivyo kufanya iwe muhimu kwa taasisi za kimataifa kubeba majukumu yao ya kihistoria katika kukabiliana na hali hii mbaya."