IRGC: Uhusiano wa kina kati ya serikali, wananchi na vikosi vya ulinzi ni dhamana ya Iran yenye nguvu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i129932-irgc_uhusiano_wa_kina_kati_ya_serikali_wananchi_na_vikosi_vya_ulinzi_ni_dhamana_ya_iran_yenye_nguvu
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeashiria umuhimu wa uhusiano wa kina uliopo kati ya serikali, taifa na vikosi vya ulinzi likiutaja kuwa muhimu kwa ajili ya kuwa na nchi yenye nguvu na iliyoendelea. Jeshi la IRGC aidha limesisitiza dhamira yake ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi na usalama kwa kuzingatia vitisho vilivyopo.
(last modified 2025-08-24T07:25:02+00:00 )
Aug 24, 2025 07:25 UTC
  • IRGC: Uhusiano wa kina kati ya serikali, wananchi na vikosi vya ulinzi ni dhamana ya Iran yenye nguvu

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) limeashiria umuhimu wa uhusiano wa kina uliopo kati ya serikali, taifa na vikosi vya ulinzi likiutaja kuwa muhimu kwa ajili ya kuwa na nchi yenye nguvu na iliyoendelea. Jeshi la IRGC aidha limesisitiza dhamira yake ya kuimarisha uwezo wa kiulinzi na usalama kwa kuzingatia vitisho vilivyopo.

Taarifa hiyo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) imetolewa leo Jumapili kwa mnasana wa Wiki ya Serikali hapa nchini inayoanza leo na kumalizika tarehe 30 mwezi huu wa Agosti kwa kukufanyika marasimu ya kumbukumbu ya kuuliwa shahidi Rais wa zamani wa Iran, Mohammad Ali Rajaei na Waziri Mkuu wa wakati huo, Mohammad Javad Bahonar. Viongozi hao wawili wa serikali walipoteza maisha katika shambulio la kigaidi mjini Tehran mwaka 1981. 

Taarifa ya IRGC imewapongeza viongozi na maafisa wote wa serikali katika shughuli hii ya wiki moja na kuitaja kuwa fursa ya thamani ya kuakisi na kutafakari kuhusu misingi ya utumishi bora na wa kujitoea uliodhihirishwa na mashahidi kama Rajaei na Bahonar. 

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran limeeleza kuwa Iran inaendelea kusonga mbele kwa uthabiti, kwa busara na uongozi wa hekima wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, mkabala na changamano za kikanda na kimataifa. 

IRGC imesema inatambua na kuthamini juhudi za serikali iliyoko madarakani kwa kushughulikia mahitaji ya wananchi na kuunga mkono vikosi vya ulinzi hasa wakati wa mzozo wa mwezi Juni mwaka huu ulioanzishwa na utawala wa Israel na Marekani. 

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pia limesisitiza dhamira yake ya kimkakati ya kuendelea kuisaidia serikali na maendeleo ya taifa na miradi ya miundombinu, likibainisha nafasi na mchango wake muhimu katika kuendeleza malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 na kuboresha masisha ya wananchi wa Iran.