Belarus yadhamiria kukuza uhusiano na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132592-belarus_yadhamiria_kukuza_uhusiano_na_iran
Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov, amesema nchi yake imedhamiria kukuza uhusiano na Iran katika nyanja mbalimbali.
(last modified 2025-10-30T12:42:34+00:00 )
Oct 30, 2025 12:04 UTC
  • Saeed Khatibzadeh (kushoto) na Maxim Tyzhenkov
    Saeed Khatibzadeh (kushoto) na Maxim Tyzhenkov

Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus, Maxim Ryzhenkov, amesema nchi yake imedhamiria kukuza uhusiano na Iran katika nyanja mbalimbali.

Ryzhenkov ameeleza haya leo alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, ambaye yuko Belarus kushiriki katika Mkutano wa 3 wa Kimataifa wa Minsk kuhusu Usalama wa Eurasia.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus ameitaja ziara ya Rais Masoud Pezeshkian wa Iran mwezi Agusti nchini Belarus kuwa ilikuwa ya mafanikio. 

Amesema ziara ijayo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran huko Minsk, ziara tarajiwa ya Rais wa Belarus mjini Tehran na ukamilishaji wa miradi ya pamoja ya masuala ya usafiri ni miongoni mwa masuala yaliyowekwa katika ajenda ya kazi ya uhusiano wa nchi mbili. 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa Iran imedhamiria kuimarisha uhusiano wa pande zote na Belarus na kuindoa vizuizi katika uwanja huo. 

Saeed Khatibzadeh ameashiria umuhimu wa uhusiano wa kistratejia kati ya nchi mbili na kusema anatumai kuwa mkutano wa kamati ya pamoja ya Iran na Belarus hapa Tehran, mabadilishano ya jumbe za ngazi ya juu na kutiwa saini makubaliano ya kimkakati kati ya Tehran na Minsk vitaimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili.