Iran na Oman zasisitiza kuimarisha zaidi uhusiano wao wa kidugu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i132628-iran_na_oman_zasisitiza_kuimarisha_zaidi_uhusiano_wao_wa_kidugu
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr Al-Busaid.
(last modified 2025-10-31T11:41:32+00:00 )
Oct 31, 2025 06:51 UTC
  • Iran na Oman zasisitiza kuimarisha zaidi uhusiano wao wa kidugu

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr Al-Busaid.

Hayo yametangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman na kuongeza kuwa mazungumzo hayo yamefanyika kwa ajili ya mashauriano kuhusu masuala tofauti.

Taarifa ya wizara hiyo pia imesema kuwa, kikao hicho cha mashauriano kati ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Majid Takht-Ravanchi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Badr Al-Busaid kimefanyika nchini Oman.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekwenda nchini humo kwa ajili ya awamu ya 11 ya mashauriano ya kisiasa kati ya nchi hizo mbili ndugu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman ameandika kwenye ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa X kuhusu mazungumzo yake na Takht-Ravanchi kwamba: Nimefurahi kukutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran. Tumejadiliana uhusiano wa pande mbili na njia za kuuimarisha, tukabadilishana maoni kuhusu maendeleo ya kikanda na kimataifa, na tukathibitisha tena uungaji mkono na ushirikiano wetu katika kutatua mizozo kupitia mazungumzo na njia za amani.