Saudi Arabia yatarajia kuwapokea kwa ukarimu Wairani wanaoshiriki ibada Hija
Saudi Arabia imetangaza kuwa imejiandaa kikamilifu kwa msimu wa Hija na inasubiri kwa shauku kuwasili kwa waumini wa Iran wanaoshiriki katika ibada ya Hija Iran, baada ya kufanya maandalizi yote muhimu ili kuhakikisha wanatekeleza ibada zao kwa usalama na faraja.
Wakati ujumbe wa Shirika la Hija la Iran ulipowasili Saudi Arabia, mwakilishi wa Wizara ya Hija na Umrah ya ufalme huo alisema kuwa kundi la kwanza la raia wa Iran wanaoshiriki ibada ya Hija mwaka hii litawasili katika mji wa Madina tarehe 25 Aprili, na kuelekea Makka baadaye kwa usalama na utulivu kamili ili kutekeleza ibada ya Hija.
Wizara ya Hija ya Saudia imeongeza kuwa inawakaribisha kwa shauku na ukarimu mkubwa wageni wa Msikiti Mtakatifu wa Masjid al‑Haram.
Mwakilishi wa Shirika la Hija la Iran pia amesema maafisa wa Saudia, katika mawasiliano kadhaa na mamlaka za Iran, wamesisitiza mara kwa mara kuwa wanawakaribisha waumini wanalenga kutekeleza Ibada ya Hija kutoka kote ulimwenguni wa Kiislamu, hasa kutoka Iran, kwa mikono miwili. Pia wameeleza kuwa maandalizi yote muhimu kuhusu malazi pamoja na usafiri wa nchi kavu, reli na anga tayari yamekamilika.
Kwa mujibu wa Shirika la Hija la Iran, takribani Wairani 30,000 wanatarajiwa kushiriki katika ibada ya Hija mwaka huu. Shirika hilo limethibitisha kuwa maandalizi ya Wairani kushiriki Hija yamefnayika kwa idhini ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.
Raia wa Iran wanasohiriki ibada ya Hija, ambao watakaa Saudi Arabia kwa zaidi ya mwezi mmoja, wanatarajiwa kutumia siku saba katika mji wa Madina.
Msafara wa kwanza wa Iran wa kuelekea Hija umeondoka mapema asubuhi katika Uwanja wa Kimataifa wa Imam Khomeini jijini Tehran.