Iran yaangamiza rada za jeshi la Marekani Magharibi mwa Asia, askari kadhaa wauawa
-
Kombora la Iran likielekea katika kambi za jeshi la kigaidi la Marekani
Majeshi ya Iran yametekeleza operesheni za uharibifu wa kina wa miundombinu kadhaa ya rada na mifumo ya mawasiliano ya kijeshi ya Marekani katika eneo hili sambamba na hujuma iliyofanya dhidi ya kambi tatu za Marekani nchini Kuwait, ikiwa ni hatua endelevu ya kulipiza kisasi dhidi ya ukiukaji unaofanywa na Marekani.
Katika taarIfa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), limefafanua kuhusu awamu mpya za Operesheni Nasr-2 (Ushindi) za IRGC na Operesheni Sa’eqeh (Radi) ya Jeshi la Iran na kusema operesheni hizo ni jibu la moja kwa moja kwa uchokozi mpya wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Katika taarifa yake ya kwanza, IRGC imesema kuwa awamu ya pili ya wimbi la 24 la Operesheni Nasr-2 imelenga miundombinu inayotumiwa katika operesheni za ulinzi wa anga za jeshi la Marekani nchini Kuwait. Jeshi hilo limeeleza kuwa awamu hii imefanyika “kufungua njia kwa kuondoa vikwazo ili kuruhusu operesheni kubwa za angani na makombora” dhidi ya shabaha za Marekani katika eneo hili.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, makombora na ndege zisizo na rubani zimelenga na kuharibu kituo cha rada cha masafa marefu, kituo cha mawasiliano, mifumo ya kupokea satelaiti, na rada ya ulinzi wa makombora inayomilikiwa na “jeshi wauaji wa watoto la Marekani” lililopo Kuwait. IRGC pia imethibitisha kuwa eneo la kuegeshea ndege zisizo na rubani aina ya MQ-9 katika Kambi ya Anga ya Ali al-Salem limeshambuliwa. Ndege kadhaa zimeharibiwa katika operesheni hiyo.
Katika ujumbe kwa taifa la Iran, IRGC imeahidi kwamba: “Operesheni ya adhabu inayotekelezwa na wana wenu [ndani ya IRGC] inaendelea.”
Katika taarifa ya pili, IRGC imetangaza kuwa imefanya shambulizi jingine dhidi ya rasilimali za ulinzi wa anga za Marekani katika Kambi ya Anga ya Ahmad al-Jaber nchini Kuwait. Taarifa hiyo imethibitisha kushambuliwa na kuharibiwa rada ya tahadhari ya mapema, mfumo wa rada wa ulinzi wa makombora, rada ya FPS-117, mfumo wa ulinzi wa anga wa Patriot, na mfumo wa mawasiliano ya satelaiti.
Baadaye, IRGC imetangaza hatua ya karibuni ya juhudi zake za kulemaza uwezo wa rada za Marekani, ikielezea shambulizi jingine ambalo “limeharibu mfumo wa rada ya ulinzi wa makombora katika kambi ya Marekani nchini Jordan na kuharibu ndege ya kivita aina ya F-15 ndani ya hifadhi yake.”
Aidha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa wanajeshi kadhaa wa Marekani wameangamizwa katika shambulizi lililolenga kambi inayohifadhi wafanyakazi wa jeshi la Marekani katika eneo la Rukban, nchini Jordan.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, IRGC imebainisha kuwa shambulizi hilo lilitekelezwa na Kikosi chake cha Anga kama sehemu ya wimbi la jipya la operesheni zake, ikiwa ni jibu la moja kwa moja kwa uchokozi endelevu wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa upande wake, Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Iran imetangaza kuwa awamu ya 19 ya Operesheni Sa’eqeh ilmeenga kambi tatu za kijeshi za Marekani nchini Kuwait, kwa kutumia ndege zisizo na rubani za kivita.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, operesheni hiyo imelenga majengo ya utawala na antena za miongozo katika Kambi ya Arifjan, eneo la maegesho ya helikopta katika Kambi ya al-Udairi, na jengo la malazi ya wanajeshi katika Kambi ya Anga ya Ahmad al-Jaber.
Jeshi hilo limesema operesheni hiyo imetekelezwa “kama jibu kwa mfululizo wa vitendo vya uchokozi na ukiukaji wa mara kwa mara wa ahadi wa ‘Shetani Mkubwa’ (Marekani).”
Katika hitimisho, Jeshi la Iran limeelezea masikitiko yake kuwa usalama wa eneo hili umekuwa hatarini kutokana na vitendo vya uhasama vya majeshi ya Marekani, ikiongeza kuwa Jeshi la Iran, kupitia makabiliano yake na Marekani, linataka kurejesha usalama na utulivu katika eneo hili.
Marekani imekuwa ikifanya ukishambulia ardhi ya Iran tangu Aprili 7, wakati Rais wa nchi hiyo Donald Trump alipotangaza usitishaji vita wa upande mmoja katika mfululizo wa karibuni wa uchokozi wa Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu. Uhalifu huo umeendelea hata baada ya Washington na Tehran kutia saini makubaliano yaliyoletwa na Pakistan mwezi uliopita, ambayo kifungu chake cha kwanza kinaamuru wazi usitishaji wa uchokozi katika nyanja zote.
Marekani pia imekuwa ikijaribu kusaidia meli kukwepa njia ya bahari iliyotengwa na Jamhuri ya Kiislamu kwa ajili ya usalama na usafiri wa kisheria kupitia Mlango-bahari wa Hormuz, kwa kujaribu kusindikiza meli zinazovamia eneo hilo kupitia njia isiyo halali. Majeshi ya Iran yamechukua hatua za kulipiza kisasi bila kusita dhidi ya kila kisa cha ukiukaji, ikiwemo juhudi za kuunga mkono harakati haramu za meli katika Lango-Bahari la Hormuz.