Rais Rouhani awatumia viongozi wa nchi za Kiislamu salamu za Idi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i15139-rais_rouhani_awatumia_viongozi_wa_nchi_za_kiislamu_salamu_za_idi
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia viongozi wa nchi za Kiislamu duniani salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa siku kuu ya Idul Adha.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Sep 12, 2016 02:36 UTC
  • Rais Rouhani awatumia viongozi wa nchi za Kiislamu salamu za Idi

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia viongozi wa nchi za Kiislamu duniani salamu za kheri na fanaka kwa munasaba wa siku kuu ya Idul Adha.

Katika ujumbe wake huo, Rais Hassan Rouhani amewatumia viongozi hao na Waislamu wote salamu katika munasaba wa Idi hii kubwa.

Rais wa Iran ameelezea matumaini yake kuwa: "Waislamu wataweza kunufaika na baraka za kimaanawi na kijamii za Idul Adha na hasa msimu wa Hija. Aidha amesema ana matumaini kuwa, kwa ushirikiano na maelewano zaidi, Waislamu wataweza kuwasilisha kwa dunia Uislamu halisi wa Bwana Mtume Muhammad SAW ambaye alikuwa msingi wa rahma na uadilifu.

Waislamu wakikumbatiana baada ya Sala ya Idi

Katika ujumbe huo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Waislamu wanapaswa kuimarisha umoja wao na kuondoa mifarakano na chuki katika umma.

Rais Rouhani amewatakia Waislamu wote duniani mafanikio katika kuimarisha misingi ya udugu na mahaba. Leo tarehe 10 Dhilhaj ni sikukuu ya Idul Adha, moja ya sikukuu kubwa za Kiislamu.

Redio Tehran inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa sikukuu hii kubwa.