Spika wa Bunge la Kenya awasili Tehran kwa ziara rasmi
(last modified Fri, 23 Sep 2016 08:07:31 GMT )
Sep 23, 2016 08:07 UTC
  • Spika wa Bunge la Kenya awasili Tehran kwa ziara rasmi

Spika wa Bunge la Kenya amewasili leo hapa mjini Tehran akiuongoza ujumbe wa nchi yake kwa shabaha ya kufanya ziara rasmi

Justin Muturi ambaye anafanya safari hapa nchini kwa mwaliko wa Dakta Ali Larijani, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amewasili leo hapa mjini Tehran na kulakiwa katika uwanja wa ndege hapa Tehran na Hossein Amir Abdollahiyan, Msaidizi Maalumu wa Spika wa Bunge la Iran katika Masuala ya Kimataifa.

Akiwa hapa nchini, Spika wa Bunge la Kenya atakutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran pamoja na maafisa wengine wa Tehran.

Bendera za taifa za Kenya na Iran

Mahusiano ya kibunge kati ya Tehran na Nairobi, matukio ya kieneo na kimataifa ni miongoni mwa ajenda kuu za mazungumzo ya Spika wa Bunge la Kenya na maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Safari ya Spika wa Bunge la Kenya mjini Tehran inafanyika katika fremu ya sera za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran za kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na nchi za bara la Afrika.

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba, inatoa kipaumbele katika siasa zake za kigeni katika suala la kuimarisha ushirikiano na nchi za Kiafrika.

Tags