Dakta Zarif: Iran inakaribisha kustawisha ushirikiano na nchi za Kiafrika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i16729-dakta_zarif_iran_inakaribisha_kustawisha_ushirikiano_na_nchi_za_kiafrika
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inakaribisha kustawisha zaidi ushirikiano wake na nchi za Kiafrika ikiwemo Sierra Leone.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Oct 05, 2016 04:31 UTC
  • Dakta Zarif: Iran inakaribisha kustawisha ushirikiano na nchi za Kiafrika

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inakaribisha kustawisha zaidi ushirikiano wake na nchi za Kiafrika ikiwemo Sierra Leone.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesema hayo wakati alipokuwa akipokea hati ya utambulisho ya balozi mpya wa Sierra Leone  Alimamy Kamara na kubainisha kwamba, sera za nje za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zinatoa kipaumbele juu ya suala la kustawisha zaidi ushirikiano na bara la Afrika. 

Kwa upande wake Alimamy Kamara balozi mpya wa Sierra Leone hapa Iran amesema baada ya kukabidhi hati yake ya utambuzi kwa Dakta Zarif kwamba, nchi yake inafuatilia kukuza zaidi ushirikiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutokana na nafasi muhimu iliyonayo nchi hii katika Mashariki ya Kati na ulimwengu kwa ujumla.

Bi Helena Sangeland, balozi mpya wa Sweden hapa Tehran akikabidhi hati yake ya utambulisho kwa Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran

Daima Iran imekuwa ikisisitiza kuwa, iko tayari kukuza na kustawisha uhusiano wake na nchi za Kiafrika katika nyanja zote hasa nchi za Kiislamu.

Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jana alipokea pia hati ya utambulisho ya Bi Helena Sangeland balozi mpya wa Swden hapa nchini Iran.