Larijan: Iran inataka kuona umoja wa kiistrataji miongoni mwa Waislamu
(last modified Sun, 28 Feb 2016 07:54:26 GMT )
Feb 28, 2016 07:54 UTC
  • Larijan: Iran inataka kuona umoja wa kiistrataji miongoni mwa Waislamu

Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu yaani Bunge la Iran amesema moja ya sera za Jamhuri ya Kiislamu ni kuona umoja na mshikamano wa kiistratajia katika ulimwengu wa Kiislamu unadumishwa.

Katika kikao na baadhi ya wabunge wa Iraqi katika mji wa Qum hapa nchini, Ali Larijan amesema Iran inaunga mkono demokrasia katika nchi zote na ndiposa imekuwa ikielezea kusikitishwa kwake na mpasuko na mgogoro unaoshuhudiwa katika nchi za Iraq na Syria, ambao amesema ni njama ya maadui ya kuvuruga amani katika eneo hili. Larijan amesema Iran haijawahi kuchochea uhasama wa kimadhehebu katika nchi za eneo hili na kusisitiza kuwa, mgogoro huo katika nchi za eneo ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na maadui wengine wa Uislamu na Waislamu.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge la Iran amewapongeza wananchi wa Iran kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge) yenye wajumbe 290 na uchaguzi wa Baraza la Wanazuoni Wataalamu Wanaomchagua Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu lenye wajumbe 88.

Kwa mujibu wa Abdolreza Rahmani Fazli, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, wapiga kura milioni 33, idadi ambayo ni sawa na asilimia 60 wa waliokuwa wametimiza masharti ya kupiga kura wameshiriki katika zoezi hilo.

Tags