Rouhani: Iran inakaribisha kuimarisha uhusiano wake na Indonesia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25734-rouhani_iran_inakaribisha_kuimarisha_uhusiano_wake_na_indonesia
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inaunga mkono kikamilifu suala la kuimarisha ushirikiano wake na Indonesia katika nyuga mbalimbali kama vile uchumi, siasa na masuala ya sayansi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 28, 2017 07:16 UTC
  • Rouhani: Iran inakaribisha kuimarisha uhusiano wake na Indonesia

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inaunga mkono kikamilifu suala la kuimarisha ushirikiano wake na Indonesia katika nyuga mbalimbali kama vile uchumi, siasa na masuala ya sayansi.

Rais Rouhani aliyasema hayo jana Jumatatu katika mkutano wake na Darmin Nasution, Waziri wa Uratibu wa Uchumi wa Indonesia na kusisitizia umuhimu wa kutekelezwa makubaliano ya pande mbili yaliyosainiwa huko nyuma kati ya Tehran na Jakarta.

Disemba mwaka jana, Rais wa Indonesia Joko Widodo aliitembelea Tehran na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa serikali ya Iran akiwemo Rais Hassan Rouhani.

Rais wa Indonesia pamoja na Kiongozi Muadhamu na Rais Rouhani Disemba 2015 mjini Tehran

Mbali na kusaini hati 4 za makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara, kadhia ya kuimarisha ushirikiano wa pamoja kati ya Tehran Jakarta katika nyanja mbalimbali ni katika masuala yaliyojadiliwa katika mazungumzo ya marais hao.

Kadhalika Iran ilisema itafanya muamala wa kibiashara na Indonesia kwa kuiuzia mafuta ghafi, gesi na bidhaa nyinginezo za petrokemikali.

Kwa upande wake, Darmin Nasution, Waziri wa Uratibu wa Uchumi wa Indonesia amesema serikali ya Jakarta inafanya kila iwezalo kuimarisha uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi mbili hizi, katika nyuga za nishati, mafuta, na miradi ya kujenga kampuni za kusafisha mafuta nchini Indonesia.