Ayatullah Jannati: Kuna haja ya kuwa macho mbele ya hatua za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26076-ayatullah_jannati_kuna_haja_ya_kuwa_macho_mbele_ya_hatua_za_marekani
Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesisitiza kuwa, kuna haja ya kuwa macho mbele ya uadui wa Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 07, 2017 23:50 UTC
  • Ayatullah Jannati: Kuna haja ya kuwa macho mbele ya hatua za Marekani

Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesisitiza kuwa, kuna haja ya kuwa macho mbele ya uadui wa Marekani.

Ayatullah Ahmad Jannati aliyasema hayo jana Jumanne katika ufunguzi wa kikao cha pili rasmi cha duru ya tano ya mkutano wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran na kuongeza kwamba, kubainisha na kueleza uadui wa Marekani kwa taifa la Iran ni jambo muhimu sana.

Ayatullah Jannati amesisitiza juu ya kutoyaamini madola makubwa na kutaka msaada kutoka kwao na kuongeza kuwa, kuna ulazima wa kutambua kuwa madola hayo makubwa ni madui wa Iran.

Mkutano wa Baraza la Wanazuoni wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu 

Mkuu wa Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran amesema kuendelea kuwa mwanamapinduzi na kufanya mambo kimapinduzi, maana yake ni kushikamana na Uislamu asili, kutetea matukufu na thamani za Kiislamu, kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na kuonyesha msimamo mbele ya maadui wa ndani na wa nje.

Mkutano wa pili rasmi wa duru ya tano ya Baraza la Wanazuoni Wanaomchagua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kusimamia kazi zake ulianza jana Jumanne hapa mjini Tehran na unatarajiwa kumalizika alasiri ya leo Jumatano kwa kutolewa taarifa rasmi.

Wajumbe wa baraza hilo Alkhamisi ya kesho watakwenda katika Haram ya Imam Ruhullah Khomeini MA mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kujadidisha baia ba utiifu wao na baadaye siku hiyo wataenda kuonana na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.