Iran yazindua kifaru cha kisasa kilichotengenezwa nchini
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26290-iran_yazindua_kifaru_cha_kisasa_kilichotengenezwa_nchini
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua kifaru cha kisasa cha kivita ambacho pia kina uwezo kutumika katika eneo lenye maji mengi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 12, 2017 10:31 UTC
  • Iran yazindua kifaru cha kisasa kilichotengenezwa nchini

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua kifaru cha kisasa cha kivita ambacho pia kina uwezo kutumika katika eneo lenye maji mengi.

Kifaru hicho ambacho kimepewa jinal la Karrar, kimezinduliwa leo Jumapili katika sherehe iliyohudhuriwa na Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein Dehqan katika kiwanda cha kutengeneza vifaru hivyo katika mji wa Doroud mkoani Lorestan.

Dehqan amesema, uundaji wa kifaru cha Karrar umechukua muda wa miaka mitatu na kwamba ni kati ya vifaru vya kisasa zaidi duniani kutokana na uwezo wake mkubwa.

Kifaru cha Karar

Amesema uwezo wa kifaru hicho wa kufyatua mizinga kwa ustadi, kubakia muda mrefu vitani na kasi kubwa ni mambo ambayo yanakifanya kifaru hicho kulinganishwa na vifaru vingine bora duniani.

Halikadhalika amesema kifaru hicho kina uwezo wa kufanya kazi usiku na mchana katika mazingira magumu ya kikazi.

Brigedia Jenerali Dehqan amesema, Iran inajitahidi kuimarisha uwezo wa magari yake ya deraya kwa kuzingatia umuhimu wa vita vya nchi kavu.