Zarif: Iran inataka kuimarisha zaidi ushirikiano na Russia
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i26962-zarif_iran_inataka_kuimarisha_zaidi_ushirikiano_na_russia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inataka kuimarisha zaidi uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na ushirikiano wa kikanda na serikali ya Moscow.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 28, 2017 08:11 UTC
  • Zarif: Iran inataka kuimarisha zaidi ushirikiano na Russia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehran inataka kuimarisha zaidi uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na ushirikiano wa kikanda na serikali ya Moscow.

Dakta Muhammad Javad Zarif ambaye anaambatana na Rais Hassan Rouhani katika safari yake nchin Russia, amesema kuwa, ujumbe wa Iran mjini Moscow unalenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi na kustawisha zaidi ushirikiano wa kikanda kati ya Jamhuri ya Kiislamu na Russia. Amesema pande hizo mbili pia zitaimarisha ushirikiano wao katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliwasili jana Moscow, mji mkuu wa Russia akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa Iran kwa ajili ya ziara rasmi ya siku mbili. Rais Rouhani anatazamiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake, Vladmir Putin hii leo alasiri. Viongozi hao wawili pia watasimamia sherehe za kutiwa saini hati na mikataba kadhaa ya ushirikiano kati ya Tehran na Moscow. 

Image Caption

Baada ya kuwasili Moscow hiyo jana, Rais Hassan Rouhani alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Russia, Dimitry Medvedev.  Alisema kuwa ana matumaini safari hii itasaidia kuimarisha uhusiano katika seta za kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na masuala ya kimataifa.