Apr 19, 2017 02:30 UTC
  • Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Walemavu wa Macho yaanza Tehran

Duru ya pili ya Mashindano ya Kimataifa ya Walemavu wa Macho yanaanza leo mjini Tehran yakiwashirikisha wawakilishi wa nchi 23.

Msimamizi wa masuala ya utamaduni ya Taasisi ya Huduma za Jamii ya Iran, Hujjatul Islam Sayyid Mahdi Sayyid Muhammadi amesema wawakilishi wa nchi za Indonesia, Algeria, Ethiopia, Pakistan, Afghanistan, Ivory Coast, Misri, Niger, Bangladesh, Lebanon, Iraq, Uturuki, Tanzania, Senegal, Nigeria, Syria, Jordan, Yemen, Togo, Cameroon na India wanashiriki katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani tukufu.  

Qarii mlemavu wa macho katika mashindano ya Qur'ani tukufu

Sayyid Muhammadi ameongeza kuwa, miongoni mwa malengo ya mashindano hayo ni kupeleka juu kiwango cha shughuli za Qur'ani tukufu katika jamii ya walemavu wa macho, kudhihirisha uwezo wa walemavu wa macho katika nyanja za kiraa na hifdhi ya Qur'ani, kuwahamasisha walemavu wa macho na kujenga uhusiano wa kimataifa kati ya vituo vya shughuli za Qur'ani vya walemavu hao.

Msimamizi wa masuala ya utamaduni ya Taasisi ya Huduma za Kijamii ya Iran amesema: Washiriki katika Mashindano ya Pili ya Kimataifa ya Qur'ani tukufu kwa ajili ya walemavu wa macho watakutana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei tarehe 27 Aprili.    

Tags