Iran yalaani hujuma za Israel nchini Syria
Iran imelaani vikali hujuma za mara kwa mara za kijeshi za utawala haramu wa Israel katika ardhi ya Syria na kusema lengo ni kuwapa nguvu magaidi wa kitakfiri Syria ambao wanaendelea kudhoofishwa kila siku na jeshi la nchi hiyo ya Kiarabu.
Akizungumza Ijumaa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi amesema hakuna shaka kuwa, hujuma hizo zinalenga kuidhoofisha serikali halali ya Syria katika fremu ya kuwapa nguvu magaidi Wakufurishaji-Wakizayuni ambao wanakaribia kuangamizwa."
Aidha amesema hujuma hizo za Israeli nchini Syria ni kinyume cha sheria za kimataifa na mamlaka ya kujitawala nchi huru ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
Siku ya Alhamisi Israeli ilihuhujumu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Damascus, mji mkuu wa Syria. Katika siku za nyuma, Tel Aviv pia iliwahi kutekeleza hujuma kama hizo ziku za nyuma.
Hujuma hizo ziliongezeka wakati magaidi wanaopata himaya ya kigeni ambao walipoingia Syria mwaka 2011.