Dec 19, 2017 13:42 UTC
  • Muirani avumbua njia ya kuwezesha kutibu ugonjwa wa Mfumo wa Neva (MS)

Mwanabiolojia Muirani, kwa mara ya kwanza duniani, amevumbua njia ya kuwezesha kutibu ugonjwa wa Mfumo wa Neva (Multiple Sclerosis) maarufu kama MS.

Mahmoud Sedaqati, mwanabiolojia Muirani akishirkiana na binti yake ambaye ni daktari, wamevumbua antigen zenye kubaini ugonjwa wa MS baada ya miaka 11 ya utafiti na hivyo kukaribia kuweza kutibu ugonjwa huo.

Akibainisha zaidi kuhusu uvumbuzi wake huo,  amesema kwa mara ya kwanza duniani sasa itawezekana kubaini uwepo wa ugonjwa wa MS kupitia vipimo vya damu.

Sedaqati ameongeza kuwa, antigen za matibabu ndio njia pekee ya kutibu ugonjwa wa MS na kuelezea matumaini kuwa, katika kipindi cha miaka minne ijayo, kutaweza kupatikana matibabu kamili ya MS.

Ugonjwa wa MS huathiri uti wa mgongo

Ugonjwa wa MS ni hatari na husababisha mwasho kwenye mfumo wa neva, yaani ubongo na uti wa mgongo. Madaktari wengi wanaamini kwamba ugonjwa huo hutokea wakati kinga za mwili zinaposhambulia chembe fulani za mwili. Kisababishi cha ugonjwa huo hakijulikani lakini inadhaniwa kwamba huenda unasababishwa na virusi. Kisha sehemu fulani za mfumo wa kinga huvamia utando muhimu wenye mafuta unaofunika nyuzi za mfumo wa neva, na hivyo kuacha makovu kwenye utando huo.

Kwa kawaida dalili huwa uchovu, unyonge, kufa ganzi kwa mikono na miguu, kushindwa kutembea, kuhisi kiu, uchungu, mwasho, matatizo ya kibofu na tumbo, na vilevile kushindwa kukuza fikira na kutofanya maamuzi ipaswavyo.

Tags