Haniya amuandikia barua Kiongozi Muadhamu akipongeza msimamo wa Iran kuhusu Quds
(last modified Thu, 18 Jan 2018 14:26:36 GMT )
Jan 18, 2018 14:26 UTC
  • Haniya amuandikia barua Kiongozi Muadhamu akipongeza msimamo wa Iran kuhusu Quds

Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemuandikia barua Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akishukuru na kupongeza msimamo wa Iran kuhusu Quds Tukufu.

Katika barua hiyo, Ismail Haniya ambaye ni Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesema taifa la Palestina linapongeza kwa dhati msimamo wenye thamani na usio na kifani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wa kuunga mkono na kuutetea mji wa Baitul Muqaddas. 

Ameshukuru msaada wa hali na mali wa taifa la Iran kwa harakati hiyo ya muqawama, chini ya muongozo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei.

Ismail Haniya amesisitiza kuwa, Quds Tukufu ni mji mkuu wa kisiasa wa taifa la Palestina na pia ni mji mkuu wa kidini wa Waislamu na wapenda haki kote duniani.

Wanamapambano wa Hamas wakiwa katika operesheni

Kadhalika ameashiria kile alichokitaja kama 'njama kuu' ya madola ya kibeberu dhidi ya Quds na Wapalestina, akisisitiza kuwa njama hizo za maadui zinalenga kuusambaratisha Ukanda wa Gaza, ambalo ni shina la muqawama na kuzima mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ili hatimaye wafanye kuwa wa kawaida uhusiano wa Israel na tawala vikaragosi za eneo hili.

Itakumbukwa kuwa, Disemba sita mwaka jana, Rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kuwa eti Quds ni mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, hatua ambayo imeendelea kupingwa kote duniani.

Tags