Rais Assad aishukuru Iran kwa msaada wake kwa Syria
Rais wa Syria ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa uungaji mkono wake kwa taifa la Syria na kusema: "Istikama ya wanajeshi Wairani na waitifaki wao katika medani ya vita ni jambo ambalo limetoa mchango mkubwa katika ushindi wa jeshi na taifa la Syria."
Rais Bashar al Assad wa Syria ameyasema hayo Jumapili mjini Damascus alipokutan na kufanya mazungumzo na Kamal Kharrazi, Mwenyekiti wa Baraza la Kistratijia la Uhisiano wa Kigeni wa Iran. Al Assad pia ameelezea matumaini yake kuwa ushindi kamili utapatikana dhidi ya magaidi katika eneo. Aidha amesema, 'iwapo Wakurdi wa kaskazini mwa Syria watafikia mapatano na serikali ya Damascus, basi eneo hilo litasalimika na satwa ya Marekani na waungaji mkono ugaidi."
Rais wa Syria pia ameongeza kuwa: "Hujuma ya kijeshi ya Uturuki Mashariki mwa Syria ni muendelezo wa uingiliaji na sera ambazo zimekuwa zikufuatwa na utawala wa Uturuki tokea mwanzo wa mgogoro wa Syria". Rais Assad amesema sera hizo za Uturuki zimejengeka katika msingi wa kuunga mkono ugaidi na makundi ya kigaidi.

Ikumbukwe kuwa Jumamosi ndege za kivita za Syria zilishambulia mji wa Afrin ndani ya Syria na oparesheni hiyo inayotekelezwa kwa kisingizi cha kukabiliana na wanmgambo wa Kikurdi ingali inaendelea.
Kwa upande wake Kamal Kharrazi amesema ushindi wa hivi karibuni wa Jeshi la Syria umepatikana kwa ushirikiano na waitifaki wake na mkondo huo unapaswa kuendelea hadi kukombolewa ardhi zote za Syria zinazoshikiliwa na magaidi. Aidha amesema maadui wa Syria na mrengo wa muqawama wataendelea na njama zao na kwa msingi huo kuna haja kwa nchi za eneo kuwa macho na kukabiliana na njama hizo.