Rais Rouhani apongeza kushiriki wananchi katika hamasa ya tarehe 13 Aban
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kufanyika Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari kunadhihisha namna wananchi walivyofungamana na walivyo na shauku na Mapinduzi ya Kiislamu na malengo yake.
Akizungumza kwenye kikao na baraza la mamawaziri jana alasiri hapa Tehran, Rais Hassan Rouhani alipongeza mahuhudhurio makubwa na ya hamasa ya wananchi katika Arubaini ya Imam Hussein (a.s) na katika marasimu ya tarehe 13 Aban; na kueleza kuwa kushuhudiwa mahudhurio makubwa kama hayo katika siku hizi mahsusi kunabeba ujumbe muhimu.
Rais wa Iran alibainisha kuwa kufanyika kwa hamasa Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari katika kipindi hiki ambapo Marekani imezidisha uadui na kujitoa kinyume cha sheria katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na katika kukaribia mwaka wa 40 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu kunadhihirisha shauku na namna wananchi walivyofungamana na Mapinduzi ya Kiislamu na malengo yake na kuwa macho na uadui wa Marekani dhidi ya taifa la Iran.
Rais Rouhani amesisitiza kuwa kushiriki kwa wingi wananchi katika marasimu ya tarehe 13 Aban kote nchini Iran kunaweka wazi kwamba licha ya kupita miaka 40 ya Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu wananchi wa Iran wangali wanafungamana pakubwa na malengo ya Mapinduzi ya Kiislamu. Marasimu ya Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari wa Kimataifa yalifanyika jana hapa Tehran na katika miji na vijiji vingine vingi hapa nchini kwa kuhudhuriwa na wananchi wanamapinduzi na wenye maono wa Iran.