Rouhani asema ugaidi, Uzayuni ni tishio kwa Waislamu duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i5182-rouhani_asema_ugaidi_uzayuni_ni_tishio_kwa_waislamu_duniani
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema ugaidi na Uzayuni ni tishio kubwa zaidi kwa ulimwengu wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 16, 2016 23:38 UTC
  • Rouhani asema ugaidi, Uzayuni ni tishio kwa Waislamu duniani

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema ugaidi na Uzayuni ni tishio kubwa zaidi kwa ulimwengu wa Kiislamu.

Rais Rouhani aliyasema hayo Jumamosi usiku alipowasili Tehran akitokea Uturuki ambapo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdogan wa nchi hiyo baada ya kuhudhuria Kikao cha 13 cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirkino wa Kiislamu OIC.

"Hali Katika ulimwengu wa Kiislamu inatulazimu tuchukue fursa ya kuwa na umoja na ili kuweza kukabiliana na vitisho vilivyopo," alisema Rais Rouhani.

Aidha amesema Iran ilishiriki kwa nguvu katika kikao cha juzi cha OIC na kuongeza kuwa Wazayuni walijaribu kuleta mifarakano miongoni mwa washiriki wa mkutnao huo wa mataifa ya Waislamu duniani.

Rais wa Iran amesema pembizoni mwa kikao cha OIC mjini Istanbul alifanya mazungumzo na viongozi wa nchi kadhaa za Kiislamu. Kuhusu mazungumzo yake na Rais wa Uturuki, Rais Rouhani amesema nchi mbili zimeafikiana kuhusu hatua za kuimarisha mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu na pia kuhusu ushirikiano wa nchi mbili hasa katika vita dhidi ya ugaidi na kukurubisha madhehebu za Kiislamu.

Kikao cha siku mbili cha 13 cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirkino wa Kiislamu OIC kilifunguliwa Alhamisi mjini Istanbul chini ya kaulimbiu ya "Umoja, Mshikamano, Uadilifu na Amani". OIC ina wanachama 57 katika mabara manne na ni taasisi ya pili ya kiserikali kwa ukubwa duniani baada ya Umoja wa Mataifa.