Waziri wa Ulinzi wa Iran: Uchokozi wowote wa adui utapata jibu kali
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i56328-waziri_wa_ulinzi_wa_iran_uchokozi_wowote_wa_adui_utapata_jibu_kali
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema chokochoko yoyote ya adui itapokea jibu kali kutoka kwa vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 29, 2019 23:48 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa Iran: Uchokozi wowote wa adui utapata jibu kali

Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema chokochoko yoyote ya adui itapokea jibu kali kutoka kwa vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu.

Brigedia Jenerali Amir Hatami aliyasema hayo jana Jumapili katika duru ya tatu ya Kongamano la Kitaifa la Jihadi na Muqawama hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, maadui wanafanya juu chini ili kulihujumu taifa la Iran.

Ameeleza bayana kuwa, "Endapo maadui watathubutu kufanya kosa na kufanya hujuma yoyote ile dhidi ya Iran basi watakabiliwa na jibu kali na la haraka."

Brigedia Jenerali Amir Hatami amesisitiza kuwa, "Hii leo ni wazi kuwa vikosi vya Jamhuri ya Kiislamu vimejitosheleza katika utenganezaji wa kila aina ya silaha, jambo ambalo linawatia kiwewe maadui."

Sehemu ndogo tu ya uwezo wa kujihami wa Iran

Ameashiria sera ya mashinikizo ya kiwango cha juu ya Marekani dhidi ya taifa hili na kubainisha kuwa, licha ya vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya wananchi wa Iran, lakini Iran ya Kiislamu inazidi kustawi katika kila nyanja. Waziri wa Ulinzi wa Iran ameongeza kuwa, "Iwapo wangelikuwa na uwezo, wangewafungia Wairani hewa ya oksijeni wasiweze hata kupumua."

Amebainisha kuwa, uwezo mkubwa wa Iran umetoa vipigo vikali kwa magenge ya kigaidi na madola ya kibeberu na hilo limetokana na taifa hili kufuata miongozo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.