Wananchi wa Iran wavunja njama za kimataifa na fitna za mabeberu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i57491-wananchi_wa_iran_wavunja_njama_za_kimataifa_na_fitna_za_mabeberu
Wananchi wa Tehran leo wamefanya maandamano ya milioni ya watu ikiwa ni kuungana na wananchi wa maeneo mengine ya Iran kulaani machafuko yaliyofanywa na wahuni wanaoongozwa na maadui wa taifa hili.
(last modified 2026-09-20T07:53:21+00:00 )
Nov 25, 2019 12:05 UTC
  • Wananchi wa Iran wavunja njama za kimataifa na fitna za mabeberu

Wananchi wa Tehran leo wamefanya maandamano ya milioni ya watu ikiwa ni kuungana na wananchi wa maeneo mengine ya Iran kulaani machafuko yaliyofanywa na wahuni wanaoongozwa na maadui wa taifa hili.

Wananchi wa Iran wameonesha kivitendo kuwa wanamuelewa vilivyo adui wa taifa lao kama ambavyo wamewathibitishia walimwengu kuwa wako pamoja na viongozi wao na ndio maana wamefanikiwa kuvunja njama za kimataifa na fitna za mabeberu.

Taarifa ya maandamano ya milioni ya watu ya wananchi wanamapinduzi wa Tehran leo Jumatatu imetangaza waziwazi kuunga mkono nguvu na usalama wa taifa la Iran. Taarifa hiyo imesema, miongozo iliyojaa busara, ya kishujaa na ya hekima ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ndiyo sababu ya kushindwa njama za kimataifa na kupelekea wananchi wa Iran wajitenge na wahuni waliochoma moto mali za umma na za watu binafsi sambamba na kuwashambulia kwa silaha moto na badiri wananchi wa kawaida na maafisa wanaolinda usalama wa wananchi hao.

Sehemu ya maandamano ya milioni ya watu mjini Tehran, Jumatatu Novemba 25, 2019 ya kulaani wafanya vujo.

 

Katika maandamano ya leo wananchi wa Tehran wametangaza kukasirishwa mno na jinai za kidhulma za maadui wenye chuki na Uislamu wanaoongozwa na Marekani na vitimbakiwiri vyao.

Taarifa ya mwisho ya maandamano ya leo Jumatatu ya wananchi hao wa Tehran vile vile imetaka kupandishwa kizimbani haraka na kupewa adhabu kali watu wote walioshiriki kwenye uhalifu wa kuharibu mali za umma na za watu binafsi humu nchini. 

Waandamanaji hao wamepiga nara kama za "Mauti kwa Marekani," "Mauti kwa Israel" na "Mauti kwa wafanya fujo" ikiwa ni kutangaza uungaji mkono wao kamili kwa juhudi za kulinda heshima, nguvu na usalama wa Iran ya Kiislamu.