Pakistan yaitaka Marekani iondoe vikwazo vyake dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i59913-pakistan_yaitaka_marekani_iondoe_vikwazo_vyake_dhidi_ya_iran
Waziri Mkuu wa Pakistan amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani aiondolee vikwazo Jamhuri ya Kiislamu hasa baada ya kuibuka virusi vya Corona.
(last modified 2026-08-14T10:24:44+00:00 )
Mar 23, 2020 03:45 UTC
  • Pakistan yaitaka Marekani iondoe vikwazo vyake dhidi ya Iran

Waziri Mkuu wa Pakistan amemtaka Rais Donald Trump wa Marekani aiondolee vikwazo Jamhuri ya Kiislamu hasa baada ya kuibuka virusi vya Corona.

Imran Khan amesisitiza kwamba, wananchi wa Iran kwa sasa wanakabiliwa na kizingiti katika juhudi za kupambana na virusi vya Corona kutokana na vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi yao.

Waziri Mkuu wa Pakistan amemtaka Rais wa Marekani azingatie masuala ya kibinadamu na kuiondolea vikwazo Iran  katika kipindi hiki cha kukabiliana na virusi vya Corona.

Imran Khan amesema katika ujumbe wake wa Twitter: Ninamtaka Rais wa Marekani Donald Trump aiondolee vikwazo Iran kwa sababu za kibinadamu mpaka pale virusi vya Corona vitakapotokomezwa.

Imran Khan, Waziri Mkuu wa Pakistan

Jana pia Russia iliitaka Marekani ikomeshe mienendo yake isiyo ya kimaadili ya kuiwekea vikwazo Iran hasa kwa kutilia maanani kipindi cha sasa cha maambukizi ya virusi vya corona. 

Licha ya kuibuka virusi angamizi vya Corona ulimwenguni ikiwemo Iran na kuweko ulazima wa walimwengu wote kukabiliana navyo, lakini Marekani ingali inang’ang’ania kuendeleza utendaji wake wa kivikwazo katika fremu ya sera za vikwazo vya kiwango cha juu kabisa dhidi ya Iran na imekuwa ikitangaza mtawalia vikwazo vipya dhidi ya Tehran

Mwenendo huu usio wa kibinadamu wa Marekani umeendelea kukosolewa na mataifa mbalimbali ya dunia ambayo sasa yanaitakka Washington ikomeshe siasa zake hizo zisizo za kiutu.