Kiongozi Muadhamu awashukuru wafanyakazi wa meli za mafuta za Iran zilizotumwa Venezuela
(last modified Tue, 09 Jun 2020 03:40:25 GMT )
Jun 09, 2020 03:40 UTC
  • Kiongozi Muadhamu awashukuru wafanyakazi wa meli za mafuta za Iran zilizotumwa Venezuela

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma ujumbe kufuatia harakati ya Kijihadi ya makamanda na wafanyakazi wa meli za mafuta za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambazo zilibeba shehena za bidhaa za petroli na kuzifikisha nchini Venezuela.

Siku ya Juamnne, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwatumia ujumbe makamanda na wafanyakazi wa meli za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema; "Nyote nyinyi azizi, manahodha na wafanyakazi wa meli za mafuta ninawapongeza kwa kazi yenu kubwa; harakati yenu ilikuwa harakati ya kijihadi na mumeifanya nchi ipate fahari."

Hivi karibuni Iran ilituma meli tano za bidhaa za petroli nchini Venezeula pamoja na kuwepo vikwazo haramu vya Marekani na hatua hii imetajwa na weledi wa mambo kuwa mafanikio makubwa kwa Iran.

Kufuatia hatua hiyo ya Iran, serikali ya Venezuela sasa imeweza kuanzisha mfumo mpya wa kusambaza petroli na dizeli nchini humo.

Meli ya mafuta ya Iran

Meli hizo tano za Iran zimefanikiwa kutia nanga nchini Venezuela pamoja na kuwepo vitisho vya Marekani vya kutumia nguvu za kijeshi kuzuia meli hizo kufika Venezuela.

Kufuatia vitisho hivyo vya Marekani, Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitahadharisha kuhusu chockochoko za Marekani katika Bahari ya Caribbean na kusema: "Iwapo meli za mafuta za Iran zitasumbuliwa na Wamarekani popote pale duniani, basi Iran nayo itawaibulia matatizo."

Meli tano za Iran zimefikisha bidhaa za mafuta kwa mafanikio nchini Venezeula na sasa ziko njiani zikirejea nyumbani. 

Tags