Zarif: Kuna upotoshaji mwingi katika hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhuisha JCPOA
(last modified Fri, 26 Mar 2021 04:35:16 GMT )
Mar 26, 2021 04:35 UTC
  • Zarif: Kuna upotoshaji mwingi katika hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuhuisha JCPOA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amejibu madai yaliyo dhidi ya Iran yanayotolewa na wakuu wa nchi za Magharibi dhidi ya Iran na kusema kuna upotoshaji mwingi kuhusu hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kuhuisha mapatano ya nyuklia ya jcpoa.

Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo Alhamisi katika ukurasa wake wa Twitter kufuatia matamshi dhidi ya Iran ambayo yametolewa na wakuu wa nchi za Magharibi kuhusu mapatano ya JCPOA. Zarif amesema: "Kuna upotoshaji mwingi sana kuhusu kile ambacho kinapaswa kufanyika ili kuhuisha JCPOA na kumefanyika jitihada za makusudi za kubadilisha mahala pa muathirika na mtenda jinai."

Zarif ameambatanisha ujumbe wake na taarifa ambayo inaonyesha hatua ambazo zimechukuliwa kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA

Taarifa hiyo ambayo imechapishwa katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ina orodha ya hatua zote ambazo zimechukuliwa kuhusu mapatano ya JCPOA tokea wakati wa kuanza rasmi utekelezwaji wake Januri 2016 hadi 25 Machi 2021.

 

Taarifa hiyo imeorodhesha hatua dhidi ya utekelezwaji JCPOA ambazo zilichukuliwa wakati wa urais wa Barack Obama na kuendelea wakati wa urais wa Donald Trump. Aidha taarifa hiyo imeashiria ukiukwaji wa JCPOA ambao umetekelezwa na utawala wa Joe Biden.

Baada ta Marekani kuchukua hatua ya upande mmoja ya kujiondoa katika mapatano ya JCPOA nchi za Ulaya zilizo katika mapatano hayo hazikutekeleza ahadi zao na hivyo, chini ya uangalizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, Iran ilianza kupunguza ahadi zake katika mapatano hayo.

Tags