Zarif: Vikwazo vyote vya serikali ya Trump dhidi ya Iran vinapaswa kuondolewa
(last modified Fri, 09 Apr 2021 13:47:41 GMT )
Apr 09, 2021 13:47 UTC
  • Muhammad Javad Zarif
    Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesisitiza udharura wa kuondolewa vikwazo vyote viilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran.

Muhammad Javad Zarif amesema leo Ijumaa katika ujumbe wake wa Twitter kwamba, vikwazo vyote vilivyowekwa na serikali ya rais wa zamani wa Marekiani, Donald Trump dhidi ya Iran, vinapaswa kuondolewa. Zarif ameongeza kuwa, Iran imeonyesha njia ya kimantiki ya kutekeleza vipengee vyote vya mapatano ya nyuklia ya JCPOA nayo ni kwamba, kwanza Marekani iliyoanzisha mgogoro huu, inapaswa kutekeleza majukumu yake yote na baadaye Iran itachukua hatua mfano wake baada ya kujiridhisha kwamba Washington imetekeleza majukumu yake. 

Dakta Zarif amesisitiza kuwa, vikwazo vyote vya Marekani dhidi ya Iran hata vile vilivyowekwa kwa kutumia majina na visingizio bandia, vinapaswa kuondolewa.

Muhammad Javad Zarif

Kikao cha pili cha Kamisheni ya Pamoja ya nchi wanachama katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kimefanyika leo Ijumaa mjini Vienna. 

Katika kikao cha leo wawakilishi wa Umoja wa Ulaya watawasilisha ripoti ya matokeo ya mashauriano ya wataalamu wa Iran na nchi wanachama katika kundi la 4+1 kwa wanachama wa Kamisheni ya Pamoja. 

Tags