May 31, 2016 04:18 UTC
  • Shamkhani: Aal Saudi wamewazuia Wairani kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema ukoo wa Aal Saud ndio uliowazuia Wairani wasitekeleze amali za Hija yenye izza na heshima.

Ali Shamkhani, ameashiria taarifa ya Taasisi ya Hija na Ziara ya Iran kuhusu kunyimwa mahujaji wa Kiirani kutekeleza amali za Hija ya mwaka huu na kueleza kuwa, ukoo wa Aal Saudi umewawekea kizuizi Wairani kutekeleza amali za Hija kwa namna sawa na ilivyokuwa katika miaka iliyopita katika mazingira ya kulindwa heshima na izza yao kama ilivyo tafsiri ya maneno hayo.

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amebainisha kuwa Hija ni wajibu na faradhi ya kidini na kuongeza kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliandaa orodha ndefu ya hatua ambazo zingeweza kuifanya serikali ya Saudi Arabia ikubali kupelekwa mahujaji wa Kiirani sambamba na kulindwa heshima, izza na usalama wao na kwamba katika kufanya hivyo ilitumia njia zote za ndani na nje ya nchi.

Utafutaji visingizio ambao umekuwa ukifanywa na Saudia kwa miaka kadhaa sasa katika sura tofauti katika uandaaji faradhi ya Hija, hatimaye umekamilika wakati wa kukaribia msimu wa Hija ya mwaka huu kwa utawala wa Aal Saud kukata uhusiano kikamilifu na Iran na mwishowe kuwazuia mahujaji wa Kiirani kuelekea katika ardhi ya wahyi kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija.../

Tags