May 06, 2022 07:41 UTC
  • Kamanda Salami: Chuki za Marekani kwa SEPAH hazina mwisho

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH amesema kuwa, chuki na uadui wa Marekani kwa jeshi hilo la Iran hauna mwisho na hakuna siku utamalizika.

Meja Jenerali Hossein Salami alisema hayo jana katika sherehe za ufunguzi wa mashindano ya Iran nzima ya Qur'ani Tukufu ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na huku akigusia uadui wa Baraza la Sanate la Marekani la kupasisha mpango wa pili wa kutoondoa vikwazo dhidi ya jeshi hilo amesema, chuki za Marekani dhidi ya jeshi la SEPAH hazina mwisho na hazitomalizika kamwe. 

Kamanda Salami amegusia pia silaha za maangamizi ya umati na msimamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwamba silaha hizo angamizi hazina nafasi katika eneo hili na kusisitiza kuwa, ni jambo lililo wazi kuwa miongozo hiyo ya Kiongozi Muadhamu ni fatwa na ni amri ya kidini ya Uislamu.

Mashindano ya Qur'ani Tukufu nchini Iran

 

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ameongeza kuwa, mwanachuoni huyo mkubwa wa Kiislamu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa tamko hilo kukabiliana vilivyo na madola ya kibeberu yaliyojirundikia silaha angamizi na hatari za nyuklia. Mwanachuoni huyu wa Uislamu ametoa fatwa hiyo ya kuharamisha silaha za nyuklia kwa kutegemea mafundisho ya Qur'ani na Uislamu yanayopiga marufuku mauaji ya watu wasio na hatia na mauaji ya umati. 

Mashindano ya 11 ya Qur'ani Tukufu maalumu kwa familia za Jeshi la SEPAH yataanza siku ya Jumapili ya tarehe 11 Mei huko Mash'had, makao makuu ya mkoa wa Khorasan Razavi, wa kaskazini mashariki mwa Iran. Sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo zilifanyika jana Alkhamisi kwa hotuba ya Meja Jenerali Hossein Salami, Kamanda Mkuu wa Jeshi la SEPAH.

Tags