Jul 09, 2022 07:41 UTC
  • Raisi: Maadui wanatumia magenge ya kitakfiri kuwagawa Waislamu

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mwenendo wa magenge ya kigaidi na kitakfiri wa kupanda mbegu za chuki na mifarakano ni sehemu ya mbinu zinazotumiwa na maadui kuibua migawanyiko katika umma wa Kiislamu.

Rais Ebrahim Raisi alisema hayo jana jioni katika mazungumzo yake na wanazuoni wa Kishia na Kisunni katika mkoa a Kurdistan, magharibi mwa nchi na kusisitiza kuwa: Maadui wanatumia magenge ya kitakfiri kuwagawa Waislamu

Ameeleza bayana kuwa, wanazuoni wa Kiislamu ni warithi wa Mitume, na hii leo wasomi hao wa Kiislamu ndio ngao kuu ya jamii mkabala wa mashambulizi tarajiwa ya maadui.

Sayyid Ebrahim Raisi amewapongeza wakazi wa mkoa huo magharibi mwa Iran kwa kusimama kidete daima dhidi ya maadui na vikosi vinavyopinga Mapinduzi ya Kiislamu.

Sayyid Raisi

Rais wa Iran amebainisha kuwa, ulimwengu wa Kiislamu umezungukwa na njama zilizopikwa na Wazayuni, Marekani na Uingereza, hivyo umma huo unapaswa kuwa macho.

Ameashiria indhari ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei juu ya njama hizo za maadui na kusisitiza kuwa, umma wa Kiislamu ulichelewa kutanabahi juu ya shari hiyo ya kuibua mifarakano baina yao.

Tags