Jul 19, 2022 08:09 UTC
  • Rais Raisi amlaki rasmi Rais Erdogan wa Uturuki mjini Tehran

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemlaki rasmi Rais wa Uturuki katika Ikuluu ya Saad Abad hapa Tehran.

Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki jana usiku aliwasili Tehran akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa nchi hiyo kwa ajili ya ziara ya siku mbili hapa nchini. Rais Recep Tayyep Erdogan wa Uturuki amelakiwa rasmi leo asubuhi na Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Iran katika hafla iliyofanyika katika ikulu ya Saad Abad hapa Tehran. 

Rais Erdogan baada ya kutua Tehran, Iran 

Hafla hiyo imefanyika sambamba na kupigwa nyimbo za mataifa mawili ya Iran na Uturuki. Rais Erdogan wa Uturuki leo alasiri atashiriki katika kikao cha Baraza Kuu la Ushirikiano wa Iran na Uturuki kitakachohuhudhuriwa pia na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.  

Uhusiano wa Iran na Uturuki utatathminiwa pakubwa katika kikao hicho cha alasiri leo sambamba na kuchunguzwa pia hatua za pande mbili za kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili.  Rais wa Uturuki aidha atashiriki katika Mkutano wa Mchakato wa Amani wa Astana kati ya Marais wa nchi tatu za Uturuki, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Russia. Katika kikao hicho cha pande tatu marais wa Iran, Uturuki na Russia watatupia jicho  matukio ya karibuni huko Syria na  mapambano dhidi ya ugaidi. 

 

Tags