Rais Raisi: Usalama na uwezo wa Iran unategemea kusimama imara wananchi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i89154-rais_raisi_usalama_na_uwezo_wa_iran_unategemea_kusimama_imara_wananchi
Rais Ebrahim Raisi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na familia ya Shahidi mlinzi wa usalama wa nchi na kueleza kwamba usalama na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unategemea kusimama imara wananchi na juhudi kubwa za maelfu ya Mashahidi, na akasisitizia umuhimu wa watu wote kuilinda na kuienzi rasilimali hiyo ya taifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 11, 2022 04:35 UTC
  • Rais Raisi: Usalama na uwezo wa Iran unategemea kusimama imara wananchi

Rais Ebrahim Raisi amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na familia ya Shahidi mlinzi wa usalama wa nchi na kueleza kwamba usalama na uwezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unategemea kusimama imara wananchi na juhudi kubwa za maelfu ya Mashahidi, na akasisitizia umuhimu wa watu wote kuilinda na kuienzi rasilimali hiyo ya taifa.

Salman Amir Ahmadi, ni mmoja wa askari shupavu wa jeshi la kujitolea la wananchi la Basij, ameuliwa shahidi na wavuruga amani katika ghasia zilizotokea katika wilaya ya 17 ya Tehran.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Rais Sayyid Ebrahim Raisi amefanya mazungumzo ya simu na familia ya shahidi huyo mlinzi wa usalama na akaeleza kwamba: rasilimali muhimu zaidi ya Iran ya Kiislamu ni wanaume na wanawake wa aina ya Shahidi Amir Ahmadi ambao kwa nyakati tofauti wanajitolea kuwa kinga na ngao za kukabili majaribu na hatari mbalimbali ili nchi na wananchi wasidhurike.
Mazishi ya Shahidi Salman Amir Ahmadi

Katika mazungumzo hayo, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya Shahidi Amir Ahmadi na kuuelezea utamaduni wa kujitolea mhanga na kufa shahidi kuwa ni miongoni mwa mambo muhimu yanayojenga nguvu za taifa la Iran na kuongeza kuwa: kile ambacho hadi sasa kimeifanya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ibaki na fahari na ushindi katika uga wa makabiliano yanayoendelea na kila aina ya vitisho, njama na vitendo vya uadui, ni rasilimali yake ya kijamii, kalima ya umoja na utamaduni wa kujitolea mhanga na kuwa tayari kufa kishahidi.

Aidha, Rais Raisi amesisitiza ulazima wa kufuatiliwa kwa uzito mkubwa tukio chungu la kuuawa shahidi Salman Amir Ahmadi.../