Jenerali Ashtari: Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i91804-jenerali_ashtari_maadui_wa_iran_ya_kiislamu_wameshindwa_kwa_fedheha
Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuegemea Jihadi ya ufafanuzi na kuweka wazi mambo katika vita vya simulizii na akasema: "Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha katika makabiliano yao na wananchi."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 17, 2022 07:39 UTC
  • Jenerali Ashtari: Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran amesisitiza juu ya ulazima wa kuegemea Jihadi ya ufafanuzi na kuweka wazi mambo katika vita vya simulizii na akasema: "Maadui wa Iran ya Kiislamu wameshindwa kwa fedheha katika makabiliano yao na wananchi."

Brigedia Jenerali Hossein Ashtari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran, Jumamosi akizungumzia fitna za hivi karibuni humu nchini amesema: "Maadui wanataka kufikia malengo yake ya kutisha na yaliyofichika katika hali yoyote ile ili kwa njia hiyo kudhuru usalama na utulivu wa wananchi na kutekeleza mpango wao wa kupindua mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran."

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Jenerali Ashtari, akizungumzia njama za hivi karibuni za maadui na watu wasioutakia mema mfumo wa Kiislamu, zikilenga zaidi vita mseto na operesheni za kisaikolojia, amesema: "Jeshi la polisi limesimama pamoja na wananchi katika uwanja wa mapambano ili kulinda na kutetea usalama na wananchi na hivyo njama za maadui zimeambulia patupu."

Waibua ghasia wanaopata himaya ya maadui wa Iran wakiteketeza moto mali ya umma na ya watu binafsi mitaani

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Iran amebainisha kuwa: "Adui ameingia kwa nguvu zake zote na kuleta kila alichonacho uwanjani ili tusiwe na Iran yenye nguvu na huru, adui anataka kuchochea tofauti za kikabila, kidini na kujitenga maeneo ya nchi, lakini ameshindwa kwa fedheha kubwa."