Marekani yaiwekea vikwazo vipya Iran, vyajumuisha Mwendesha Mashtaka Mkuu
Wizara ya Fedha ya Marekani imeiwekea Iran vikwazo vipya kwa kisingizio cha ukiukaji wa haki za binadamu, katika kuendeleza uingiliaji wake wa masuala ya ndani ya Iran na kutekeleza sera ya mashinikizo ya juu zaidi dhidi ya Tehran.
Tangu yalipoanza machafuko nchini Iran, serikali ya Joe Biden haijaacha kuchukua kila hatua huku ikieleza kinagaubaga kwamba badala ya kujikita kwenye mazungumzo na muelekeo wa kidiplomasia ambao imekuwa ikiupigia upatu kila mara, itafuatilia zaidi machafuko yanayojiri Iran.
Washington imeamua pia kuendeleza sera za mashinikizo ya juu kabisa za utawala wa Donald Trump; na kwa ushirikiano wa waitifaki wake wa Magharibi, hadi sasa imeshaiwekea Iran vikwazo kadhaa kwa kisingizio cha haki za binadamu ili kuunga mkono machafuko yaliyojiri nchini.../