May 02, 2023 01:33 UTC
  • Shamkhani asisitiza kuanzishwa utaratibu wa matumizi ya Riyali na Rupia

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ametilia mkazo kuanzishwa utaratibu wa kutumia sarafu ya Riyali na Rupia katika mabadilishano ya kibiashara na kiuchumi kati ya Iran na India.

Ali Shamkhani Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran jana alikuwa na mazungumzo hapa Tehran na Ajit Doval Mshauri wa usalama wa Taifa wa Waziri Mku wa India ambapo alibainisha kuwa: Uhusiano imara wa nchi mbili za Iran na India hauathiriwi na matakwa ya upande wa tatu na si dhidi ya upande wowote. Shamkhani aidha ametaka kuanzishwa utaratibu ambapo sarafu ya Iran ya Riyali na Rupia ya India zitatumika katika mabadilishano ya kiuchumi baina ya nchi mbili. 

Iran na India na mkakati wa kutumia sarafu za taifa katika mabadilishano ya biashara 

Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran ameeleza kuwa: Masuala ya pamoja ya  ustaarabu, historia na utamaduni mkongwe kati ya pande mbili, azma ya viongozi wa nchi hizo na pia uhuru wa kistratejia wa Iran na India ni misingi mikuu iliyopelekea kuimarika ushirikiano wa pande mbili.   

Shamkhani ameongeza kuwa: Matukio ya kimataifa na kikanda  yameandaa mazingira mazuri ya kuimarishwa ushirikiano kati ya  Iran na India katika nyanja za nishati, usafirishaji na tranziti, teknolojia na masuala ya benki kati ya nchi mbili.

Katika mazungumzo hayo, Ajit Doval Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Waziri Mkuu wa India ameeleza kuwa: Nchi huru duniani zinapasa kujiandaa kwa ajili ya kustawisha ushirikiano wa kikanda na kuwa na mchango chanya kimataifa kwa kutambua sifa za matukio ya dunia na wakati huo huo kuimarisha uwezo wao wa ndani.

Tags