Iran haitamtuma balozi mpya Uswidi kufuatia kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini humo
Duru katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran zinadokeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeamua kutomtuma balozi mpya nchini Sweden kutokana na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Scandinavia.
Kwa mujibu wa tovuti ya Press TV, hayo yamedokezwa Jumapili, siku nne baada ya raia wa Sweden kukanyaga nakala ya Qur'ani Tukufu na kisha kuiteketeza moto nje ya msikiti mkuu wa Stockholm chini ya usimamizi wa polisi.
Kitendo hicho cha kufuru kilikuwa kimeidhinishwa na polisi wa Uswidi kwa kisingizio cha sheria za uhuru wa kusema.
Ijapokuwa taratibu za kiidara zimekamilika za kumtuma balozi mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sweden, Wizara ya Mambo ya Nje kwa sasa haina mpango wa kumtuma mwanadiplomasia huyo mpya nchini humo kutokana na kutokana na kuvujiwa heshimadhidi ya Qur'ani Tukufu. chanzo cha habari kilisema.
Uchomaji moto wa kukufuru wa Kurani, ambao uliambatana na kuanza kwa Eid al-Adha ya Waislamu mwishoni mwa Hija ya kila mwaka ya Hija, ulizusha wimbi la hasira na lawama katika ulimwengu wa Kiislamu.
Siku ya Alhamisi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ilimwita balozi mdogo wa Uswidi katika mji mkuu Tehran na kumkabidhi malamiko makali ya Iran kuhusu kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu katika nchi hiyo ya Ulaya.
Wakati wa kikao hicho, mkurugenzi mkuu wa wizara hiyo katika ukanda wa Ulaya Magharibi alimwambia mwanadiplomasia huyo wa Uswidi kwamba kitendo hicho cha matusi ni mfano wa chuki na mwelekeo wa uchokozi ambao umetekelezwa kwa kutumia vibaya kanuni ya uhuru wa kujieleza.
Afisa huyo wa Iran alisema kwamba, kimya cha Stockholm kimewatia moyo wale waliokiuka moja ya kanuni za kimsingi na za wazi za haki za binadamu, yaani kanuni ya kuheshimu maadili ya kidini na ya Mwenyezi Mungu.
Aghalabu ya serikali za nchi za Waislamu pia zimepinga dharau na utovu wa adabu uliofanyika huko Sweden dhidi ya Quran Tukufu. Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Imarati imemkalisha kiti moto balozi wa Sweden nchini humo na kusisitiza kuwa, hatua ya serikali ya Uswidi ya kuwaruhusu watu wenye misimamo mikali kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu ni kielelezo cha kutoheshimu maadili ya kijamii.
Sekretarieti ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) pia imetangaza kuwa, itaitisha mkutano wa dharura wa jumuiya hiyo wiki ijayo katika mji wa Jeddah, Saudi Arabia, kwa lengo la kuchunguza dharau na kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden.