Wapenzi wa Qur'an kukusanyika ubalozi wa Sweden Tehran kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i99470-wapenzi_wa_qur'an_kukusanyika_ubalozi_wa_sweden_tehran_kulaani_kuvunjiwa_heshima_qur'ani
Wadau mbalimbali wa Qur'an leo watakusanyika katika ubalozi wa Sweden mjini Tehran kulaani kuvunjiwa heshima Qur'an tukufu huko nchini Sweden.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jul 02, 2023 23:20 UTC
  • Wapenzi wa Qur'an kukusanyika ubalozi wa Sweden Tehran kulaani kuvunjiwa heshima Qur'ani

Wadau mbalimbali wa Qur'an leo watakusanyika katika ubalozi wa Sweden mjini Tehran kulaani kuvunjiwa heshima Qur'an tukufu huko nchini Sweden.

Taarifa zaidi zinasema, wanaharakati wa Qur'an wakiwemo wakurugenzi, walimu wa Qur'ani, maqarii na mahufadhi leo Jumatatu watakusanyika mbele ya ubalozi wa Sweden hapa mjini Tehran kwa ajili ya kukemea na kulaani kitendo cha kishenzi cha kuvunjiwa heshima Qur'an tukufu huko Sweden.

Jumatano mchana tarehe 28 mwezi Juni raia wa Sweden aliyejukana kwa jina la Salwan Momika (37) alichoma moto na kuchana nakala ya Qur'ani Tukufu huko Stockholm mji mkuu wa nchi hiyo katika siku ya kwanza ya Sikukuu ya Idul-Adh'ha. Momika alitenda jinai hiyo baada ya polisi wa Sweden kumpa kibali cha kufanya maandamano dhidi ya Uislamu. Kabla ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu, Momika aliweka nyama ya nguruwe kwenye nakala ya kitabu hicho kitukufu, ambayo ni ishara ya kukidunisha na kukivunjia heshima kupitiliza kwa waumini wa dini ya Kiislamu. 

 

Baadhi ya nchi za Kiislamu zikiwemo Pakistan, Uturuki na Yemen pia sambamba na kuendelea kulaani kitendo hicho cha kishetani cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu nchini Sweden, zimetaka kususiwa bidhaa kutoka Sweden.

Siku ya Ijumaa waandamanaji wenye hasira mjini Baghdad wamvamia ubalozi wa Sweden mjini humo kulalamikia kitendo cha kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Sweden na kutaka kutimuliwa mjini humo balozi wa taifa hilo la Ulaya.

Mahakama ya Rufaa ya Sweden iliruhusu maandamano ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu, kwa kubatilisha marufuku ya awali ya polisi dhidi ya maandamano hayo. Uhalifu huo mkubwa umendelea kulaaniwa vikali ya Waislamu kote duniani.